Namna ya Kujiunga na Kozi
Kujiunga na Kozi
Kujiunga na kozi yoyote unayoipenda kwenye Karakana app ni rahisi na huchukua hatua chache tu. Fuata maelekezo haya:
Hatua ya 1: Kuanzisha Muamala
- Fungua ukurasa wa Maelezo ya Kozi unayotaka kujiunga nayo.
- Angalia maelezo ya kozi, bei yake (Mfano: Tsh 10,000), na mwalimu wake.
- Bofya kitufe cha Jiunge Sasa kilicho kwenye ukurasa. Hii itakupeleka kwenye ukurasa wa malipo.
Hatua ya 2: Kuchagua Njia ya Malipo
Ukurasa wa Malipo utakuonyesha maelezo ya bidhaa/kozi unayolipia na utaombwa kuchagua njia ya malipo.
- Chini ya sehemu ya Njia ya Malipo, gusa kwenye sehemu ya kuchagua na uchague mtandao unaotumia kwa ajili ya malipo.
- Unaweza kuchagua Airtel Money au Tigo Pesa.
Hatua ya 3: Kukamilisha Malipo
Baada ya kuchagua njia ya malipo, sehemu ya kuingiza nambari ya simu itaonekana.
- Nambari ya Simu: Ingiza nambari ya simu ya mtandao uliyouchagua ambayo ina salio la kutosha.
- Bofya kitufe cha: Lipa Sasa
Baada ya kubofya Lipa Sasa, utapokea ujumbe mfupi wa (USSD prompt) kwenye simu yako ukiomba Nywila (PIN) ili kuthibitisha muamala. Ingiza Nywila yako kwa usahihi ili kukamilisha malipo.
Bofya Thibitisha malipo ilikuthibitisha malipo yako.
Ikiwa malipo yako yameshindikana, tafadhali jaribu tena au wasiliana na huduma kwa wateja kwa msaada zaidi.
Hatua ya 4: Kusoma
Kozi zote ulizo nunua zinapatikana kwenye ukurasa kwa Akaunti yangu. Utachagua kozi ulio nunua na kuendelea Kusoma kwa kubonyeza Endelea kusoma





