Ruka hadi maudhui makuu

Namna ya Kujiunga na Wakufunzi

Kujiunga na Timu ya Wakufunzi wa Karakana

Unaweza kujiunga na Karakana kama mkufunzi na kuanza kushiriki ujuzi wako kwa jamii. Fuata hatua hizi muhimu.

Hatua ya 1: Kukamilisha Wasifu

Kabla ya kutuma maombi, ni lazima uhakikishe kuwa taarifa zako za msingi za wasifu zimekamilika.

  1. Kwenye ukurasa wa Akaunti, bofya Hariri Wasifu.
  2. Jaza taarifa zote zinazohitajika:
    • Jina la kwanza na Jina la mwisho.
    • Tarehe ya Kuzaliwa na Jinsia.
    • Namba ya simu.
  3. Hakikisha unapakia picha ya jalada (cover photo) na picha ya wasifu (profile photo).
  4. Bofya Hifadhi Mabadiliko.

Hatua ya 2: Kuanzisha Maombi

  1. Rudi kwenye ukurasa wa Akaunti yangu.
  2. Bofya kadi ya Jiunge na wakufunzi wetu.
taarifa

Kumbuka: Ikiwa wasifu wako haujakamilika, mfumo utakuelekeza kurudi kwenye ukurasa wa Hariri Wasifu (Hatua ya 1).

Hatua ya 3: Kujaza Fomu ya Taarifa za Ziada

Ukibofya kitufe cha kujiunga, utaelekezwa kwanza kujaza fomu ya taarifa za ziada za mtumiaji kwa ajili ya takwimu zetu.

  1. Jaza taarifa kama Aina ya makao yako, Mkoa, na Kiwango cha Elimu.
  2. Jibu maswali kuhusu ulemavu na kama wewe ni mkimbiiz.
  3. Bofya Wasilisha Fomu.

Hatua ya 4: Kujaza Fomu ya Maombi ya Mkufunzi

Baada ya kuwasilisha Fomu ya Taarifa, utaelekezwa kwenye Fomu ya Maombi ya Mkufunzi ambayo inahitaji maelezo ya kitaaluma:

  1. Jaza taarifa zako za Taarifa Binafsi (Nchi, Cheo chako, Wasifu wa kitaaluma/Bio).
  2. Jaza maelezo ya Uzoefu na Motisha:
    • Uzoefu wako wa Kufundisha.
    • Sababu (Motisha) za kutaka kufundisha.
    • Mada Unazopendelea kufundisha.
  3. Bofya Tuma maombi.

Hatua ya 5: Kufuatilia Hali ya Maombi

  1. Baada ya kutuma maombi, utarejeshwa kwenye ukurasa wa Akaunti yangu.
  2. Unaweza kufuatilia hali ya maombi yako (Mfano: INASUBIRI) kwenye sehemu ya Hali ya Maombi.
  3. Uhakiki wa maombi huchukua 3-5 siku za kazi. Utapokea taarifa pindi maombi yako yatakapoidhinishwa au kukataliwa.