Namna ya kujisajili
Hatua ya 1: Kukubali Vigezo na Masharti
Kabla ya kuendelea na usajili, unahitaji kukubali sheria na masharti yetu.
- Tafuta na soma kwa makini Vigezo na Masharti yalipo chini ya vitufe vya kujisajili.
- Weka alama ya tiki kwenye kisanduku kuashiria kuwa unakubali masharti hayo yote.
Hatua ya 2: Usajili
Baada ya kukubali masharti, Unaweza kujisajili aidha kwa kutumia barua pepe tako ama kwa kutumia akaunti yako ya google.
- Usajili google
- Usajili kwa barua pepe
- Bonyeza G Jisajili kwa google
- Chagua Account unayotaka kusajilia.
- Baada ya kuingiza nambari ya uthibitisho kwa usahihi, utakuwa umeingia moja kwa moja!
- Sasa unaweza kuanza kutumia Karakana na kuanza kujifunza masomo unayoyapenda.
Hatua ya 1: Kujaza fomu.
- Jaza taarifa zinazohitajika:
- Majina kamili: Ingiza jina lako lote.
- Barua Pepe (Email): Ingiza anwani ya barua pepe unayotumia.
- Nywila (Password): Chagua neno la siri lenye nguvu. Unaweza kubofya jicho dogo upande wa kulia ili kuona au kuficha nywila.
- Thibitisha Nywila: Ingiza neno la siri hilo hilo tena ili kuthibitisha kuwa umeiingiza kwa usahihi.
- Baada ya kujaza sehemu zote, bofya kitufe cha: Jisajili
Hatua ya 2: Uthibitisho wa Barua Pepe (Email Verification)
taarifa
Mara tu utakapo bofya Jisajili, barua pepe yenye nambari ya uthibitisho itatumwa kwenye anwani ya barua pepe uliyojaza.
- Fungua Sanduku lako la Barua Pepe.
- Tafuta barua pepe kutoka Kreative Karakana.
- Haujapata Barua Pepe?
- Angalia Spam/Junk Mail: Huenda barua pepe ikawa imeingia kwenye kikasha cha spam au junk mail, hakikisha umeangalia huko.
- Thibitisha Anwani: Hakikisha unatumia sanduku la barua pepe lililo sawa ambalo uliliingiza kwenye Hatua ya 2.
- Nakili nambari ya uthibitisho uliyotumwa.
- Rudi kwenye Karakana app na ingiza nambari hiyo kwenye sehemu inayohusika kikasha bonyeza Thibitisha.
Hatua ya 3: Kuingia na Kuanza Kujifunza
Baada ya kuingiza nambari ya uthibitisho kwa usahihi, utakuwa umeingia moja kwa moja!
- Sasa unaweza kuanza kutumia Karakana na kuanza kujifunza masomo unayoyapenda.


